DSpace Repository

Lugha na Uvumbuzi wa Kisayansi na Kiteknolojia.

Show simple item record

dc.contributor.author Muusya, J. K.
dc.date.accessioned 2023-03-29T10:43:56Z
dc.date.available 2023-03-29T10:43:56Z
dc.date.issued 2023-03
dc.identifier.uri http://repository.kyu.ac.ke/123456789/929
dc.description.abstract Uvumbuzi kimsingi huwa unahusisha utambuzi wa vitu, hali na hali aambazo zilikuwapo awali lakini zikawa ama hazijulikani au hazikuwa zimetambuliwa kwa kupewa majina. Utambuzi huu hutumia lugha. Huku nikusema kuwa uvumbuzi niutambulishaji wakitu ambacho hakikujulikana kikajulikana. Ni uwasilishaji wamawazo kupitia uwazaji makinifu. Kwa kuwasilisha mawazo na maoni, wavumbuzi huwa wanatambulisha kitu kwa kutumia lugha. Uwazaji unaotumia lugha huwapa wavumbuzi uwezo wa kufikia taswira za kindani zilizojisetiri kwenye bongo zao. Wanasayansi makini hutumia lugha kuunda upya mawazo na maoni yao upya ili kuenda nana muktadha wa changamoto zinawasukuma kuvumbua. Suala hili huzua mtiririko wamawazo ambao hujengeka kwenye mawazo yao yaawali yaliyokuwa kwenye akilizao. Kwa hivyo ni wazi kwamba ili kufikia maarifa yoyote mapya katika uvumbuzi nisharti kutumia lugha. Kutokana na nafasi kubwa ya lugha katika uvumbuzi, inakisiwa kuwa umadhubutiwa sera ya lugha katika taifa lolote nirutuba ya uvumbzi wa wanasayansi. Katika uchunguzi huu, tunajiuliza, wanasayansi huvumbua chochote kipya au huwa wanatumia lugha kutambulisha jambo, kitu, maarifa au mawazo yaliyokuwapo tayari? Na je, kipi cha msingi zaidi katika uvumbuzi, sayansi au lugha? Ikiwa uvumbuzi huandamana na kuwezeshwan alugha, je mwanasayansi yoyote anapaswa kuitwa mwanaisimu? Na je, sera ya lugha katika mataifa ya Afrika inaathiri uvumbuzi? Maswali haya ndiyo tutashughulikia katikautafiti huu. Uchanganuzi nauhakikiwa nafasi ya lugha katika uvumbuzi wakisayansi na kiteknolojia utafanywa katika utafiti unao kusudiwa. Matokeo ya utafiti huu yatatumiwa kupendekeza kwawashika dau kuimarisha sera ya lugha katika bara la Afrika kama njia ya kuendeleza uvumbuzi. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher 6th Annual International Conference-2023, Kirinyaga University, Virtual en_US
dc.subject Lugha, Uvumbuzi, Sera ya lugha, Wanasayansi na Wanaisimu en_US
dc.title Lugha na Uvumbuzi wa Kisayansi na Kiteknolojia. en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account